FURAHA YA KUZALIWA KWANGU.
Hakuna mwema kama wewe muumba wangu,
Uliyeniwezesha kuifika siku yangu,
Ni siku ya leo siku ya kuzaliwa kwangu,
Umeniepusha mengi na kuniondoshea machungu,
Ukanipa nguvu na kuimarisha afya yangu,
Hukuweka siri ukabainisha wabaya wangu,
Ukaficha na kuzistiri aibu zangu,
Ewe mola waridhie na wasamehe wazazi wangu,
Wape afya njema kama ulivyofanya kwangu.
-
"...
Kwenye dunia inaenda
isiwe kwenye wewe unaenda.
..."
#_Ibra's Diary 32-
Society part 1
This generation imekua direction-less,
Caption ya RIP inafatwa na funny meme, emotionless,
Mapenzi kwa streets inaongozwa na vijana, pointless,
Si mtaachana tu imekua headline, aimless,
Focus imeshift from kuogopa pregnancy na kuchunga diseases, hopeless,
Wazee after years of marriage wamechokana sasa wamekua sponsors, shameless,
Siasa imekua biashara, kushiba na kuziba uchi,
Kutumikia nchi imegeuka kutumia nchi,
-
Mama♥️... Part 1
Unakumbuka zile bidii aliweka,
Early morning digging someone's acre,
At least a provide kale ka-fee shule,
Ajaribu pia kuziba kale ka kiraka on your uniform,
Unakumbuka ukijaribu kusoma na koroboi ili shule uperform,
Alicheza Chama ya wamama, akiwa na leso moja ya akiba,
Hiyo ndio ilikua ya harusi, graduation na pia ya msiba,
Aling'ang'ana kwenda bookshop to get you books,
Not forgeting trying to make your hair for good looks,
Your mama tried to give you her all,
She deserves your hand now when she gets to fall,
She deserves your support now that she's aging,
Alienda on her knees and cried, praying,
Ili Sir God akulinde ukue mkubwa, just saying,
...
-
Lini niliwahi kukulaumu eeh Mungu?
Na ni lini nitafanya hivyo?
Na kwanini nifanye hivyo?
Kamwe!
Vyote utoavyo,
Vyote uchukuavyo,
Ni kazi ya Mikono yako,
Na kazi yako ni Neema,
Kwetu.
Wanifanya nitabasamu ninapopokea,
Na ninapopoteza wanifanya jasiri,
Wanifanya mwenye nguvu ninapoanguka,
Kufuta mavumbi na kushinda vyote.-
You can do it!
Motivation occurs everyday,
Unaamka asubui na unarealise God's great, unasali for a successful day,
Your dreams keep pushing you kila siku,
Hustle ata ikiwa ngumu aje unai embrace mchana na usiku,
Inasemekana mtafuta hachoki,
Kesho utapata gas ili uache kupigana na kuni, moshi,
Ila hustle ni kitu haifai kustop,
Piga mandazi surwa leo kesho Utakula pizza na smokie,
Joy comes in the morning though unaamka na miayo,
Ila kubali hali kwa sababu everyday is a new opportunity to make it better, na si njaro,
Kulalamika haitakutoa kwa situation poor,
Being courageous na kuset goals itakuset kwa levels kubwa,
Ukianguka, kubali, lakini amka ju una kibali,
No one knows how tomorrow turns out,
Fanya your best na uache Mungu afanye the rest,
Usi develop kiburi, hiyo inakam before a fall,
Kua na roho nzuri, smile and be happy kama kipa aliyeshika Ball,
You can do it!-
Tumia mafanikio ya wenzio kama hamasa kwako kutimiza malengo; utabarikiwa kadiri unavyowabariki wengine na utajilaani kadiri unavyowatakia mabaya wenzio. Kumbuka: "Roho mbaya haijengi"
-
Ni bora kuishi na mama mzazi ambaye anakupenda kwa dhati na anajivunia uwepo wako hapa duniani na ana amini wewe ni damu yake na mungu atakulipa kwa hilo,kuliko kumpenda mtu anayejifanya anakujua zaidi ya mama yako na ukiondoka ana kuramba kisogo.
Nakwambia
"Usinidanganye upendo wa mama hauna mfano"-