Ibrahim Sultan   (MshairiMpole)
78 Followers · 38 Following

POETRY MAN IN ZANZIBAR,TANZANIA FROM EAST AFRICA
+255715160597
Joined 24 July 2018


POETRY MAN IN ZANZIBAR,TANZANIA FROM EAST AFRICA
+255715160597
Joined 24 July 2018
1 DEC 2021 AT 11:50

Radhi naitaka kwako pale nilipo kosea,
Kuyachosha macho yako Jumbe hii kupokea,
Labda ni nia yako hapa mwisho kufikia,
Hayo ni mawazo yako miye sijayatambua,
Ni miye kipenzi chako mpenzi wa hii dunia,
Nakupenda peke yako wallaahi nakwambia,
Nataka huko uliko dua njema kunombea,
Na nikawe mume wako pia mke wangu pia.

-


24 AUG 2021 AT 13:21

Si Kila aendae na asirudi basi eti amepotea katika safari yake hiyo,Bali wengine hujipanga ni jinsi gani ya kurudi na kuanza upya safari yake hivyo huchukua muda kujipanga upya ili Kuleta mabadiliko,Utofauti na ushindani.

-


23 AUG 2021 AT 19:41

1.BINADAMU ALIVYO
Ukinyamaza ukamuacha afanye atakavyo basi atajishtukia na aseme humpendi kisa humkosoi na kumwambia lolote,
Ukizungumza na kumwambia ni jinsi gani hupendezwi na kila baya afanyalo atakwambia unamfatilia sana na humpi nafasi/Uhuru wa kufanya atakayo pia.

-


7 APR 2021 AT 14:52

SICHOKI
Tazama ninaandika na sichoki kukwambia,
Taratibu si haraka kwamba nakunyenyekea,
Penzi hili la hakika si uongo nakwambia,
Kwako mi Sina mashaka wazi nimekuridhia,
Najiona nimefika macho yameziba njia,
Sitaki kwako kutoka Penzi kulitumikia,
Ewe wangu muhibaka miye nakunyenyekea.

-


3 APR 2021 AT 16:17

NATESEKA
Nateseka kwa hamu ya kukuona,😔
Tafarijika kwa penzi lako liso hiyana,😔
Sitafika kilele cha kukupenda sana,😔
Tataabika pale tutakapo kwaruzana,😔

kipi ninachojivunia zaidi ya Pendo lako?💝
nani wa kuzidia miye nasema hayupo,💁‍♂️
Sijamuona Mwengine aliye zaidi yako,🙅‍♂️
Nawaza nikikuona na kulia papo hapo,😢
Furaha nitayopata nitakisi shavu lako.💋

-


27 MAR 2021 AT 11:55

Kazi moja kubwa ya viongozi mashuhuri ni kuota ndoto kubwa,
kiongozi usiku unapolala unaota maslahi mapana ya wananchi,
kiongozi mzuri ni yule anayeota mambo makubwa kwa maslahi ya wananchi wake.
Lakini kuna viongozi wengine wanaota mambo yao binafsi wengine wanaota mambo makubwa lakini hawayatekelezi sasa John Pombe Magufuli alikuwa akiota na anatekeleza na ndiyo maana ndoto yake bado ni endelevu hakika shujaa wa Afrika tutakukumbuka JPM.

-


18 MAR 2021 AT 2:38

Tanzania tumefiwa,Mioyo inaumia,
Jama tumeondokewa,Tunalia Tunalia,
Kiongozi alokuwa,Leo kajiondokea,
Si kwamba aliamuwa,Ni mola kamchukua,
Jemedari Msifiwa,MAGUFULI alikua,
Jama tumeondokewa,Tanzania Tunalia.

-


5 MAR 2021 AT 11:52

Wapende wale wasio kupenda ili iwe ni nasaha za ukarimu wako.

-


27 FEB 2021 AT 22:18

Fanya kila kinachotokana na wewe basi kiwe ni Miongoni mwa MAWAIDHA tosha kwa wote Wanaokuzunguka na iwe ni SWADAQA ya kuitengeneza njia yako ya milele.

-


23 FEB 2021 AT 11:37

Lisikuchomozee jua Hali ya kuwa umo midomoni mwa watu kwa uovu wako,jizuie kwa kila aina ya kiungo chako kusababisha makereko kwa mwenzako
kwa kufanya hivyo utakuwa umejisalimisha mbele ya muumba wako.

-


Fetching Ibrahim Sultan Quotes