Misemo ya wenye hekima iliyo kusanywa pamoja na mwenye busara mmoja ni hazina isiyo isha .
-
Kila mji ufikiwa kwa njia yake , kadhalika kila jambo ufanyika Kwa namna yake.
-
Kama fahari ya jua linapo pambuzuka asubui , ndivyo ilivyo fahari ya kijana anaye tembea kwa busara wakati wa ujana.
-
Dhahabu ya kweli utaipata kwa wachimba madini, kadhalika na kuhusu habari za maisha waulize wazee.
-
mwenye busara uonekana tangu mwanzo, na ata akiwa mbali ana tambulika.
-
Ata mashauri yaweza kutoweka kwa wenye busara, na ata hekima ya weza kupotea Kwa mtu.
-
Ni taishi Kwa ajili yangu mwenyewe hadi lini ?
Ulichonipa nikwa ajili yangu mimi na wewe ,
Je, nitawatazamia wengine lini ?-
Tafakari za mtu mbaya umuongoza kutenda mabaya na tafakari za mtu mwema umuongoza kutenda mema.
-
Ngazi ina hatua fupi fupi sana , ila ndizo zinazo mfikisha mju juu kadhalika vitu vidogo vidogo vikikusanywa pamoja hakika yake vitakuwa vingi.
-
Mwenye busara utazama, kisha ujifunza kwa makosa ya watu wengine, na kuanguka Kwa wengine kwake ni huzuni.
-