QUOTES ON #KISWAHILI

#kiswahili quotes

Trending | Latest
17 OCT 2021 AT 15:38

Kamba Isipokatikia Pembamba Tutapatwa Na Wasiwasi,
Tutaanza Kutazamana Usoni Tukitafuta Wa Kumlaumu.
Huyu Atadhani Ni Yule Amesababisha
Yule Atamsingizia Huyu Ameikata.
Kamba Isipokatikia Pembamba Tutaanza Kupatafuta Panene Ilipokatikia
Pengine Tutagundua Panene Hapakuwa Panene
Ni Macho Yetu Tu Yalitulaghai,
Pengine Palikuwa Ni Panene Kweli
Lakini Ni Kwa Wakati Huu Tuu Kamba Imeamua Ikatikie Panene.

Dunia Haiachi Kustaajabisha!

-


13 MAY 2019 AT 20:50

TAFAKARI MURUA
Hakuna matokeo mengine utakayoyapata baada ya
"kuikaza kamba kwa kutumia nguvu zako"
Zaidi ya kamba hiyo kukatika tu na mwishowe kuilaumu mikono na nguvu zako wakati mungu alikupa ubongo wa kufikiria kabla ya kufanya jambo lolote lile.
@ebrehiem7

-


22 JAN 2022 AT 21:10

SITAKUACHA SALAMA!

Kama Nikifa Kwa Sababu Ya Mapenzi Yako Sitakuacha Salama.
Nitakufuata Kwenye Kila Ndoto Zako,
Na Kila Usingizi Wako.
Nitahakikisha Unapata Mateso Na Mahangaiko Ya Kutosha,
Ukiniacha Sitakuacha Hivihivi Tu,
Maisha Yako Yatakuwa Tamthiliya Ya Ujasusi Kwangu!

Ukitaka Kupenda Mwingine Nitahakikisha Hufanikiwi,
Kama Nikipoteza Uhai Kwa Sababu Ya Kukupoteza Wewe,
Nitaiba Na Moyo Wako Ili Usije Kupenda Mwingine Tena,
Nitahakikisha Unatambua Thamani Yangu Iliyopotea!

Kama Ikitokea Hunitaki Tena Nitaendelea Kukutaka Kimoyomoyo,
Hata Katika Usingizi Wa Kifo Nitakuja Kukutisha Ndotoni.
šŸ˜‚šŸ˜‚ Aise! Usije Thubutu Kuniacha
Kwa Kuwa Ukiniacha Sitakuacha Salama! šŸ˜‚šŸ˜
Sio Kwamba Nakutisha, Nakupa Tahadhari Tu.

Bruno DS Daniel

-


30 MAR 2020 AT 13:40

Natamani ningekuwa hakimu

Nawe uwe kitabu cha sheria Kesi kuisimamisha

Basi hata ningekuwa wako mwalimu

Kanuni za mapenzi ningekufundisha

Mwandani wangu wewe ni mkarimu

Wangu moyo wautakatisha

Kila nionapo Lako tabasamu

Furaha yangu unaizidisha

Nitakupenda daimaa....

-


23 SEP 2021 AT 13:24

UNAPOTEA
Kwa Udogo Wa Akili Yako Unadhani Tabasamu Huashiria Furaha

Kwa Uhaba Wa Maarifa Ulionao
Umejipambanua Kwa Kuwaiga Wengine

Katika Upofu Wa Moyo Wako
Umeijenga Amani Kuwa Anakupenda Wewe Pekee!

Katika Upungufu Wa Imani Yako
Umejiaminisha Ndugu Hawawezi Kuwa Marafiki Unaokutana Nao Maishani

Katika Mtindio Wa Ubongo Wako
Umebaki Ukiabudu Uzao Usio Kuzalia Matunda.

Kwanini Uwe Na Wasiwasi?
Wakati Kwa Upungufu Wa Utashi Wako Umeshindwa Kutambua Jinsi Wakujali Vyo Wale Wanao Kuzunguka.

Maisha Yako Yamekuwa Yako Peke Yako
Taabu Shida Na Furaha Zako Zimebaki Katika Umimi Wako..

Katika Upweke Ulionao Maishani Mwako
Umeijenga Dunia Yako Unayoishi Peke Yako..

.. Rafiki, Unapotea.

-


19 MAR AT 16:01

~Nitarudi
Nitarudi simulia, uzuri wa Afrika
Urembo wa Malkia, sifa zake Bi Malika
Barawa ya Somalia, hadi pwani Tanganyika
Nitarudi hadithia, ngano zilothibitika

Nyumbani peke sikia, nitarudi kuandika
Wa kwetu si Arabia, wasifu wa kusifika
Sauti ya kuvutia, nyoka akadhihirika
Tenzi kuzifurahia, kwenye mizani ya sika

Jua litapofifia, na kiza kutufunika
Mawimbi yakatulia, pepo zikatamatika
Muda utapowadia, na beti kukamilika
Nitarudi simulia, yale niliyoandika

-


8 OCT 2021 AT 1:47

USIHANGAISHWE NAO
.....
Wanakaa Wanakuteta Gizani
Wanafurahi Na Wewe Kukikucha
Wanashindwa Kukushusha Kwa Kuwa Hawajui Huko Kileleni Ulifika Je.
Muumba Wa Mbingu Na Ulimwengu Yuko Pamoja Nawe
Wasikutishe, Kamwe Usihangaishwe Nao.
....
Kwa Nini Unahangaika Kutafuta Thamani Mbele Ya Macho Yao Yaliojaa Upofu .
Wao Katika Wingi Wao Hawamfikii Huyo Mmoja Uliye Naye Katika Umoja Wake
Alivyo Navyo Huyo Mmoja
Ndivyo Wasivyo Navyo Hao Wengine Unaodhani Wanaweza Kuwa Mbadala Wake
Hakukosea Kuwa Na Huyo Uliye Naye
Moyo Huchagua Katika Maono Yake
Wala Si Macho Katika Kutokuona Kwake
Wala Si Masikio Katika Kutokusikia Kwake
Tulia Hapo Ndipo Unapostahili Kuwepo
Hao Wengine Ni Wa Kupita
Kamwe Usihangaishwe Nao.
....
Maisha Yana Mambo Chungu Nzima Sio Lazima Uwe Na Ufahamu Wa Yote
Kwa Maana Kujua Mengi Kwa Juu Juu Ni Hatari
Ni Kheri Kuyajua Machache Kwa Kina.
Hayo Mengine Uso Yajua Yasikusumbue
Jikite Katika Hayo Unayo Yaweza
Maneno Ya Wajuaji Kamwe Usihangaishwe Nayo
Kwa Maana Pana Tofauti Ya Karama Lakini Kwa Mungu Wote Sisi Ni Sawa.
........
Sakalani, Bruno D.

-


8 JAN 2022 AT 0:23

HALELUYAAH!

Haishangazi Leo,
Ulivyovaa Si Sawa Na Jana
Umependeza Leo,
Kuliko Ulivyovutia Juzi.
Na Kila Unapoongea Sauti Yako Ni Tulizo,
Na Kila Unapocheka Vicheko Vyako Ni Furaha Kwangu.
Kwanini? Kwanini Nisifurahie Uwepo Wako?
Macho Yangu Yakikuona Yanatamani Yaendelee Kukutazama,
Masikio Yangu Yakikusikia Hayawezi Yakaacha Kukusikiliza.
Ladha Uliyoileta Kwenye Maisha Yangu Haielezeki,
Vilivyokuwa Ugali Sasa Ni Biriani!
Palipokuwa Pamepa Suka Wewe Umepaziba
Kwangu Umekuwa Kithibitisho Kuwa Yapo Maji Yanayoweza Kuzoleka Yakimwagika!
Haleluyaah!

Bruno DS Daniel

-


6 DEC 2021 AT 1:15

Siku Kupenda Kwa Kuwa Nilikosa Wa Kunipenda,
Sikuzama Kwenye Penzi Lako Kwa Kuwa Eti Nilihitaji Ukaribu Nawe.
Hapana,
Sikukimbilia Kwako Kwa Kuwa Eti Nilihitaji Kukombolewa,
Nilifanya Yote Ili Tu Nipate Kuusikia Moyo Wangu Ukidunda Kwa Mara Nyingine Tena.

Kama Ulidhani Wewe Ni Mkombozi Wangu Unajidanganya,
Sikuhitaji Uwe Mkombozi Wangu Nataka Uwe Mpenzi Wangu,
Nataka Uwe Na Mimi Pale Ambapo Nakuhitaji,
Nataka Unipende Mno Kama Ninavyo Kupenda Sana.

Hili Swala La "Mkombozi" Linapaishwa Sana
Lakini Unaweza Ukawa Kama Ikikupendeza
Lakini Kwangu Mimi Sihitaji Mkombozi
Nahitaji Mpenzi Wa Kupunguza Uzito Wa Mizigo Yangu.

-


31 OCT 2021 AT 15:13

UKITAKA KUKATA ROHO!

Bado Tunakuhitaji
Katika Ubora Wako Uliweza Kuyafanya Mengi Yaliyo Tuvutia Sisi Na Wengine Wengi
Bado Tunataka Na Tunahitaji Kuwa Na Wewe
Umuhimu Wako Kwetu Hauelezeki
Hivyo Utakapotaka Kukata Roho Uyakumbuke Mengi Utakayoyaacha Hayajakamiliwa
Ukumbuke Sisi Tunao Kuombea Upata Ahueni
Ukumbuke Familia Yako Inayotamani Urudi Nyumbani Ukajumuika Nao
Na Sisi Tunaendelea Kuomba Kwa Mungu Akuponya Kama Yatakuwa Ni Mapenzi Yake.

Usisita Kutuita
Hatuondoki Tupo Hapo Nje.
Ukitaka Kukata Roho Mkumbuke Tena Mungu Katika Ukimya Wa Roho Yako
Sauti Zetu Zina Litaja Jina Lako Madhabahuni
Tuna Imani Mungu Atatenda Vile Yeye Inampendeza.

Kama Ni Sasa Au Badaye Ukitaka Kukata Roho Tafuta Namna Utajulisha
Tulipotoka Na Wewe Ni Mbali
Kuanzia Urafiki Sasa Tumekuwa Familia Moja.

Mipango Ya Mungu Kwetu Wanadamu Hatupaswi Kuielewa
Hata Tukijaribu Tutaishia Kupotoka
Tunatakiwa Tuipokee Kwa Kuwa Ni Yeye Mungu Pekee Ndiye Anayejua Sababu Ya Hili Na Lile Kutokea
Hivyo Hata Sasa Unapokata Roho
Tunamshukuru Mungu Kwa Kuwa Mapenzi Yake Yametimizwa
Machozi Yanayotoka Machoni Mwetu Yanatukuza Ufalme Na Uwezo Ulio Tukuuka Wa Mungu Mwenyezi.
.....................

-