11 NOV 2019 AT 12:53

NAKUPENDA
Elewa Hisia zangu kwako wewe kuwa mimi nakupenda,
Kwako nimefika na Upofu nitapotea siniache ndia panda,
Sina Mwengine zaidi yako kwengine mi sitakwenda,
Maradhi umenitia kwako miye ni mgonjwa meniwatia kidonda,
Jibu lako ndio dawa basi nipe tafadhali sinipatie kalenda,
Usinitese afya yangu yadorora tazama ninavyo konda.

- MshairiMpole