HAYA MAISHA!
Maisha ni mfano wa muandaaji wa mapambano ya ngumi aliye na wapiganaji na ulingo wake mwenyewe uitwao dunia.
Mwanadamu aliyejaliwa mwenye mpumzi huingia kwenye ulingo huu kupambana.
Kwenye mapambano ya maisha utapambana na wapiganaji tofauti tofauti wenye mbinu mbalimbali; mmoja mmoja au hata kwa pamoja!
Mapambano haya hayakwepeki na wala huchagui mpinzani. Uchaguzi ni wako kupigana au kurudisha pumzi kwa aliyekupa!
#Nawazatu 🤔- Nsajigwa_jr
29 MAY 2022 AT 22:09