Adier Palmer   (𝕃𝕦𝕓𝕒𝕟𝕘𝕒)
136 Followers · 101 Following

I was born to write experiences and feelings
Joined 8 February 2018


I was born to write experiences and feelings
Joined 8 February 2018
15 MAR AT 16:58

A polite notice to anyone
wishing to block me this year.

Kindly make sure it's
IRREVERSIBLE.


If you can't stand my negatives
Don't stand my positives also.
If you can do a day without me
Make it a lifetime decision too.
Life must continue...

It's time to unhung me
from your horrible life

|2024|


-


8 MAR AT 9:22

One thing personally najua
Ni that our love ni maua
Na hakuna kitu kitayaua
Leave alone kukuchukua

It's so deep, doo haziwezi nunua
Na kwa madem soo bado nitakuchagua
Heri nipoteze rada kama Gachagua
Juu wakileta noma, maneno nitafyatua

Halafu sahi nikama nishajua
Hii yote ni Mungu amejibu dua
Siamini ati ni mimi ushaamua

Sitaki mchanga uingie kwa kitumbua
Kama vile ilimess love ya Wambua na Kambua
Kwa hizo deepfaked videos akimnyandu***

Babe, I know kuna day hii love itakua
So sweeter than avocado na muwa
Na tena perfect, juu rohoni ushatua

We're here to stay, hiyo niko sure
Hata kama itamean kuishi kwa mashua
Juu kwa jangwa langu wewe ndio mvua
Hiyo tena ninaswear, nikisema niko sure
Kama bet, nimerisk juu najua niko sure


|4-U|

-


20 FEB AT 18:22

ANA DAMU YA KUNGUNI

Jiulize ni kwa nini,uanzapo kuongea,
Sana sana makundini,watu hukuondokea,
Ndugu ujitathmini,hakika umepotea,
Sisi tuwakuombea,mwenye damu ya kunguni!

Mwenye damu yakunguni,nayo Lugha ya ajuza,
Wengi hawamtamani,maneno yake yaliza,
Yeye ana walakini,dosari kuliko pweza,
Kama wewe umefunza,sote hutuona duni!

Sote hutuona duni,na hilo tumezowea,
Kazi zetu zote guni,yeye tu amebobea,
Umewachokoza mbuni,mateke atapokea,
Sisi tuwakuombea,upae hadi hewani!

Upae hadi hewani,ujione kama bingwa,
Mewashinda gazetini, wandishi kwako wapingwa,
Yeye qwetu mpinzani,metia mipaka tingwa,
Twakwombea mtafiti,hesabu hadi mizani!

Hesabu hadi mizani,utunge kwa kukosoa,
U hodari hesabuni,nasi tushakuzoea,
We nduli kwa majirani,na waja mekutegea,
Kurekebisha hajui,ywatwanika peupeni!

Ywatwanika peupeni,ywajisifu mjuaji,
Amezidi zetu mboni,na amejivunjia mji,
Twamwachia waamuzi,kesi wasome majaji,
Sisi tuwakuombea,sirekebike kidogo!


|Kimelea|

-


8 FEB AT 19:23

Hiliyambo limekithiri,alifanyao haoni,
Nalisema nami si siri,limechacha kanisani,
Naona litanawiri,mapema mlikomeni,
Wanadada walokole,tunzeni waume wenu!

Walalama kilamara,eti nyinyi hamweshimu,
Mwajiletea madhara,na pia mwajihukumu,
Wa kanisa ndi vinara,la waume hamweshimu,
Wanadada walokole, tunzeni waume wenu!

Kija kwako mhubiri,kabati walifungua,
Hadi wapanda kwa dari,sahani nzuri watoa,
Mfanyavyo si vizuri,badilisheni tabia,
Wanadada walokole, tunzeni waume wenu!

Wanaume wazunika,Kila muda kanisani,
Nyumbani na waboeka,mfanyapo na kuhani,
Nyoyoni wasononeka,boma lao mabadini,
Wanadada walokole, tunzeni waume wenu!

Wacha mume kafurahi,muishini kwa neema,
Ndoa yenu tamirihi,mtachekelea wema,
Kitazama tanabahi,mtasifiwa salama,
Wanadada walokole, tunzeni waume wenu!

Safari nazo punguza,mrembeshe wako mume,
Najua nimewaguza,mume siye paka shume,
Yeye atauguuza, moyo wako usikwame,
Wanadada walokole, tunzeni waume wenu!

Rekebisheni nasihi,ndoa ziache vunjika,
Someni wangu nasihi, mbeleni nawapeleka,
Nasaha Nimewaahi,ndoa na hazitavunjika,
Wanadada walokole, tunzeni waume wenu!


|Wanadada walokole|

-


3 FEB AT 15:00

ATAKUWA MAMA MTU

Nina wangu chautamu,'kiwa naye naridhia
Yeye kwangu ni muhimu,kaniteka kihisia
Kwake hainishi hamu,daima anivutia
Atakuwa mama mtu,nami niwe baba mtu.

Huyu ndo kichaa wangu,napenda wazimu wake
Namuelewa kivyangu,tangu mie aniteke
Sitaki atoke pangu,moyo wangu uteseke
Atakuwa mama mtu,nami niwe baba mtu.

Kwake mie ni mhuni,apenda usela wangu
Nyumbani ndo maskani,pazuri sio pachungu
Kazi yake kijiweni,kuzichana ndevu zangu
Atakuwa mama mtu,nami baba mtu.

Yeye kwangu mhubiri,injili yake yatamba
Kauli zake ni nzuri,haziboeshi zabamba
Kwake hali kweli nzuri,hatujawahi kulumba
Atakuwa mama mtu,nami baba mtu.

Kwake nimekuwa teja,sina mwendo asilani
Kaniteka mwenye tija,niko 'high' jamanini
Hoja ninazoboboja,sizielewi wendani
Atakuwa mama mtu,nami niwe baba mtu.

Kwangu amekuwa mwizi,ameniiba mzima
Na tena mchana wazi,kabla jua kuzama
Aniita laazizi,natoa kutu 'mi chuma
Atakuwa mama mtu,nami niwe baba mtu.

Kwangu amekuwa mama,mtoto nadekadeka
Kutwa ananitazama,nisiweze kudhurika
Hapa kweli nimefuma,ndege simwachi hakika
Atakuwa mama mtu,nami niwe baba mtu.

-


3 FEB AT 7:15

MAZIWA YALITIWA NINI ?

Wakazi wa Budalangi,nazo nne zote wodi,
Ninayo maswali mengi, nayasema bila hodi,
Kunaye likuja wingi,katupa nyingi baridi,
Maziwa litiwa nini,ama yalitiwa ndimu?

Asubuhi kawa freshi,jioni yakawa mala,
Yakapewa ushawishi,yanywe kabla kulala,
Yana zuri nunukishi, Budalangi katawala,
Maziwa litiwa nini, ama yalitiwa ndimu?

Tukaona ndiyo bora,yatatupa ahueni,
Maziwa kawa karara,yakadhimu madhumuni,
Kawa dawa ya kuhara,yakawa safi tumboni,
Maziwa litiwa nini, ama yalitiwa ndimu?

Leo hino nashangaza,ndiyo mwiba matumboni,
Yanatufanya kuwaza,tulo fikiri zurini,
Tena hakuna kwangaza,twayaona kisogoni,
Maziwa litiwa nini, ama yalitiwa ndimu?

Kwani yalituwa ndimu,na yule tu mtawala,
Ama kipi kilidumu,hapa nyumbani Bunyala?
Sijataja muhudumu,ila meunda muwala,
Maziwa litiwa nini, ama yalitiwa ndimu?

Swali langu mujibuni, akilini linitoke,
Nitulize mtimani, moyoni sihangaike,
Jawabu ndo natamani, jamani sihuzunike,
Maziwa litiwa nini, ama yalitiwa ndimu?

-


26 JAN AT 8:20

Random thoughts

1. Be happy for what you have
while working for what you want

2. Be healthy and take care of yourself, but be
happy with the beautiful things that make you, you.

3. "People say that money isn't the key to happiness,
but I always figured if you have enough money,
you can have a key made."


|Happiness|

-


20 JAN AT 22:40

VIPI NIMEBAHATIKA

Urembo nayo akili, kwako hani ni zawadi
Mpole sio mkali, wanipendeza zaidi
Unafikiria mbali, huyawazii ya jadi
Mimi nimebahatika, kwani 'mekupata wewe.

Wewe ni mrembo ndani, na nje wala sisemi
Faragha na hadharani, najipigia ukemi
Nyonda mkalia ini, milele uishi nami
Mimi nimebahatika, kwani 'mekupata wewe.

Nakupenda kila siku, tulivyo sisi ni bora
Mechi tunacheza peku, mipira wadaradara
Hamna anokupiku, tikitaki zako bora
Mimi nimebahatika,kwani 'mekupata wewe.

Nimekuwa nimejua, ma'na halisi ya penzi
Ni ba'da ya kukujua, nilipozama penzini
Lako linasisimua, wanimaliza kimanzi
Mimi nimebahatika, kwani 'mekupata wewe.

Wewe kwangu romantic, nabakia zumbukuku
Chizi mie sishiriki, wanisoma kama 'buku'
Kesini watoa haki, bila kutumia chuku
Mimi nimebahatika, kwani 'mekupata wewe.

Sauti yako lahani, yatoa nyoka pangoni
Maneno yako laini, yagusa vyote mwilini
Tabasamulo usoni, lavutia sana hani
Mimi nimebahatika, kwani 'mekupata wewe.


Ni vipi nimebahatika?

-


19 JAN AT 23:26

MWANANGU RUDI NYUMBANI

Nimesikia mwanangu, mji umekulemea,
Umeyapata machungu, furaha ikapotea,
Ila hujafungwa pingu, ukashindwa kurejea,
Mji ukikulemea, mwanangu rudi nyumbani,

Nyumbani kunalo shamba, njoo ufanye zaraa,
Upande hata migomba, ndizi iweze kuzaa,
Uache zenu kasumba, zinazo- wapeni njaa,
Mji ukikulemea, mwanangu rudi nyumbani,

Mji usikusumbue, kwa fikira za chakula,
Leo mboga ununue, kesho njaa utalala,
Huku mboga ununue, utaonekana fala,
Mji ukikulemea, mwanangu rudi nyumbani,

Mjini kodi walipa, huku ukiwa na nyumba,
Na urithi nimekupa, nyumba pamoja na shamba,
Mwanangu nyumbani hapa, hapana kuyumbayumba,
Mji ukikulemea, mwanangu rudi nyumbani,

Kuna mengi sijasema, yakupayo matatizo,
Sitaki kutematema, moyoni yawe mzozo,
Ila nasema mapema, kwako niwe yako nguzo,
Mji ukikulemea, mwanangu rudi nyumbani


Haya maisha ya mjini
Ni maisha ya majini

-


25 NOV 2023 AT 12:32

Kuna time nilikuwa nastay Kasa
Hizo time nilikuwa nazunguka tao ka saa
Nilikuwa mbiggy manze ka sir
Hujaienda place na ukaambiwa kaa sir
Juu ya kuwa point out perfectly Cursor
Zilikuwa tu mablessings si Curse ah
Living large and driving flashy Cars ah
wajaka wakidai niko na pesa yaani "cass" a


|Lyrical|

-


Fetching Adier Palmer Quotes